Posts

Showing posts from December, 2017

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva anazidi kubeba vichwa vya habari kutokana na kasi na mchango wake anaozidi kuutoa katika klabu yake ya Difaa El Jadid. Simon Msuva kwa mara ya pili anafanikiwa kuifungia timu yake goli muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Morocco, Msuva jana ameipatia ushindi wa goli 1-0 timu yake ya Difaa El Jadid dakika ya 52 dhidi ya Hassania Agadir. Kufunga kwa goli hilo kunamfanya Simon Msuva kusogea katika msimamo wa ufungaji bora kwani goli dhidi ya Agadir limemfanya kutimiza jumla ya magoli 5 na mtu anayeongoza ana magoli saba lakini huu ni mchezo wa pili kwa Msuva kufunga mfululizo

New York yaimarisha ulinzi katika mkesha wa mwaka mpya itakayofanyika kwenye uwanja wa Times

Idara ya polisi ya New York imeimarisha ulinzi wakati wa mkesha wa mwaka mpya utakayofanyika kwenye uwanja wa Times. Idara hiyo imesema itaongeza ulinzi nje ya uwanja huo ili kuhakikisha ulinzi dhidi ya magari kwa watu wanaosubiri kuingia kwenye eneo la ukaguzi. Aidha, polisi na washirika wengine wa usalama wataongeza idadi ya vituo vya ukaguzi kote katika uwanja wa Times ili kusimamia maeneo yanayofaa kuangalia maonyesho uwanjani hapo. Kila mwaka, karibu watu milioni mbili wanakwenda kwenye uwanja wa Times kujumuika kwenye mkesha wa mwaka mpya.

Vigogo wamiminika kurejesha fomu

Image
 IKIWA leo ndiyo siku ya mwisho kwa viongozi wa umma, kuwasilisha fomu za kuonyesha rasilimali mbalimbali walizonazo katika Ofi si za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wabunge na wakuu wa wilaya ‘wamemiminika’ katika Ofi si za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam kuwasilisha fomu hizo. Miongoni mwa viongozi waliofika na kuwasilisha fomu zao ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe; Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe; Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema; Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Harold Nsekela alisema kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa viongozi mbalimbali wanaofika katika ofisi hizo katika kanda zote na kuwasilisha fomu...

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (Tewuta) kimepongeza hatua ya Rais John Magufuli kumtaka Waziri wa Fedha kuanza uchunguzi kubaini ukweli kuhusu ubinafsishwaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Katibu Mkuu wa Tewuta, Junus Ndaro amesema chama hicho kinatambua fika kuwepo mchezo mchafu uliosababishwa na Watanzania wachache wenye uchu wa fedha wakisaidiana na wawekezaji kupora rasilimali hiyo ya Taifa. Ndaro amesema leo Alhamisi Desemba 28,2017 kuwa, kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa kikitoa malalamiko kuhusu ufisadi huo serikalini lakini hakikusikilizwa.   “Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuthubutu kutamka pasipo shaka kuwa taarifa alizonazo zinaonyesha kampuni ya Airtel ni mali ya TTCL, jambo hili tulilipigia kelele kwa muda mrefu,” amesema. Ndaro amesema mara zote hawakusita kutamka kuwa Celtel ambayo sasa ni Airtel ni mali ya TTCL iliyoporwa pasipo kulipwa chochote. “Wafanyakazi tunatambua ku...

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

Image
  Polisi mkoani Kilimanjaro inamshikilia mfanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF) kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Anitha Oswald (32). “Askari wakiwa doria walimkamata Anitha Oswald, ambaye ni mkazi wa Karanga, Manispaa ya Moshi, akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 216 na gramu 370 kwa kutumia gari lake analomiliki aina ya Toyota Sienta rangi ya silva,” alisema kamanda Issah. Kamanda Issah alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Majengo kwa Mtei Desemba 19 akitokea Njia Panda ya Himo kuchukua mzigo huo. “Jeshi la polisi mkoani hapa liko makini, operesheni inaendelea na hatutamvumilia mtu yeyote ambaye atabainika kujihusisha na biashara hii”, alisema. Kamanda huyo alisema polisi wanaendelea kumtafuta dereva wa gari hilo ambaye alikimbia baada ya kulitelekeza lilipogonga mti wakati akiwakimbia askari.

Shirika la ndege la Ethiopia lafikiria kuanzisha safari za kwenda Zhengzhou, China

Shirika la ndege la Ethiopia linafikiria kuanzisha safari za kwenda mji wa Zhengzhou, China. Mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya China, Mongolia, na Korea ya Kaskazini Bw Yared Berta, amesema mpango wa kuanzisha safari za kwenda mji wa Zhengzhou, Mkoani Henan China, ni sehemu ya jitihada za kuwavutia wateja wapya. Bw Berta amesema mji wa Zhengzhou ni moja ya sehemu zinazojulikana nchini China, ambao unavutia uwekezaji mwingi, na kutoa fursa kwa shirika la ndege la Ethiopia haswa kwenye huduma za uchukuzi wa mizigo. Hivi sasa Shirika la ndege la Ethiopia linasafirisha abiria 80,000 na tani 60,000 za mizigo kila mwaka kupitia miji tano ya China, ambayo ni Beijing, Hongkong, Shanghai, Chengdu na Guangzhou.

Umoja wa mataifa watoa mwito wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo yenye migogoro

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF limetoa mwito kwa pande mbalimbali zinazopambana kutekeleza wajibu wa sheria za kimataifa na kukomesha mara moja ukatili na mashambulizi dhidi ya watoto. Mkurugenzi wa miradi ya dharura wa UNICEF Bw. Manuel Fontaine amesema watoto wanalengwa na kuwekwa kwenye mazingira ya kufanyiwa ukatili mkali majumbani kwao, mashuleni na kwenye maeneo wanakocheza. UNICEF imesema watoto wamekuwa shabaha ya mstari wa mbele, na kutumiwa kama ngao, wanauawa, wanalemazwa na kuajiriwa kupigana katika sehemu mbalimbali duniani. Shirika hilo pia limesema vurugu za kingono, ndoa za lazima, utekaji nya ra na utumwa yamekuwa ni mambo ya kawaida kwenye migogoro ya Iraq, Syria, Yemen, Nigeria, Sudan Kusini na Myanmar.

Rais wa Russia autambua mlipuko wa St. Petersburg kuwa shambulizi la kigaidi

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, mlipuko uliotokea jumatano kwenye supamaketi moja mjini St. Petersburg nchini humo ni shambulizi la kigaidi. Rais Putin ameagiza Idara ya usalama FSB kuwakamata magaidi haraka iwezekanavyo, na kwamba endapo maofisa wa usalama watakabiliwa na hatari ya maisha kwenye operesheni ya msako, wamepewa mamlaka ya kuwaangamiza magaidi papo hapo bila haja ya kuwakamata hai.

Mti uliopandwa miaka 200 iliyopita katika Ikulu ya Marekani kukatwa

Image
Mti wa kale ambao umekuwepo Ikulu ya Marekani kwa karibu miaka 200 utakatwa. Mti huo unaofahamika kama "Jackson" magnolia ulipandwa na rais Andrew Jackson kama kumbukumbu kwa mke wake. Umekuwa ukionekana kwa picha wakati wa sherehe nyingi huko White House na hata picha zake ziliwekwa kwenye noti za dola 20 kati ya mwaka 1928 na 1988. Lakini wataalamu wanasema kuwa mti huo umeharibiwa na kuwa hatari kwa usalama. Mke wa Trump Melania Trump Msemaji wa White House Stephanie Grisham anasema Bi Trump alichukua hataua hiyo kwa sababu mti huo ulikuwa ni tisho kwa usalama wa wageni na waandishi wa habari ambao mara nyingi husimama mbele yake wakati helikopta ya rais inapaa. Mtu wa Magnolia ulipandwa kutoka ya mti wa magnoalia uliokuwa ukipendwa na Rachel Jackson katika shamba lao huko Tennessee. Marais 39 wamehudumu mti huo ukiwa White House na pia ulikuwepo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani na vita vya kwanza na vya pili vya dunia. ...

MAVUNDE AWATAKA POLISI JAMII KUUNDA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Image
Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde amewataka Vijana ambao wanashiriki katika mafunzo ya Ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato. Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma. “Pamoja na jukumu kubwa mlilonalo na ulinzi na usalama wa raia na mali zao,lakini pia mhakikishe mnatumia mkusanyiko wenu kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujiongezea kipato na kutengeneza nafasi za Ajira zaidi,”amesema Mavunde amewataka vijana hao kuyatumia vyema mafunzo waliyopata kwa kuwa waadlifu,waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kusimama mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa na AMANI na UTULIVU. Naye, Kamanda wa Mkoa wa  Polisi wa Dodoma,SACP  Gilles Muroto amewataka Vijana zaidi kujitokeza katika Ulinzi shirikishi ili kui...

Biashara kati ya China na nchi za nje yatarajiwa kuzidi dola za kimarekani trilioni 4 katika mwaka 2017

Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje itazidi dola za kimarekani trilioni 4 katika mwaka 2017, na itaendelea vizuri na kwa utulivu katika mwaka 2018. Ripoti iliyotolewa leo na wizara ya biashara ya China imesema, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje katika miezi 11 iliyopita ya mwaka 2017 imefikia dola za kimarekani trilioni 3.7, ambacho iliongezeka kwa azilimia 15.6 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

Umoja wa mataifa watoa mwito wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo yenye migogoro

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF limetoa mwito kwa pande mbalimbali zinazopambana kutekeleza wajibu wa sheria za kimataifa na kukomesha mara moja ukatili na mashambulizi dhidi ya watoto. Mkurugenzi wa miradi ya dharura wa UNICEF Bw. Manuel Fontaine amesema watoto wanalengwa na kuwekwa kwenye mazingira ya kufanyiwa ukatili mkali majumbani kwao, mashuleni na kwenye maeneo wanakocheza. UNICEF imesema watoto wamekuwa shabaha ya mstari wa mbele, na kutumiwa kama ngao, wanauawa, wanalemazwa na kuajiriwa kupigana katika sehemu mbalimbali duniani. Shirika hilo pia limesema vurugu za kingono, ndoa za lazima, utekaji nyara na utumwa yamekuwa ni mambo ya kawaida kwenye migogoro ya Iraq, Syria, Yemen, Nigeria, Sudan Kusini na Myanmar.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita nchini Jamhuri ya Kongo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali ya Jamhuri ya Kongo na kundi la upinzani linaloongozwa na Pastor Ntumi. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Stephane Dujarric, inasema katibu mkuu anaelezea matumaini kwamba makubaliano hayo yanasaidia kuleta utatuzi wa amani na endelevu wa vita katika eneo la Pool la nchi hiyo na kupunguza msukosuko wa kibinadamu huko. Eneo la Pool la nchi hiyo ni eneo la kusini linaliozalisha mafuta ikiwa ni pamoja na mji mkuu Brazzaville. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia pande hizo mbili kutekeleza makubaliano hayo.

Chegeni aanza kutoa 'tiba' ya vyuma kukaza

Image
MBUNGE wa Jimbo la Busega Dk. Raphael Chegeni amewataka vijana na akina mama jimboni Busega kuacha kubweteka na kudai vyuma vimekaza bali waongeze bidii kwa kuchapa kazi kwa nafasi ya kila mtu mmoja mmoja na ndani ya vikundi vyao. Ushauri huo ameutoa wakati akikabidhi vifaa vya kumwagilia maji mashambani kwa ajili ya kikundi cha vijana wa Hapa Kazi Tu Busega cha Nyanhanga na fedha taaslimu shs Milioni 1, kwa kikundi cha Inuka mama cha Nyashimo. “Hii ni changamoto kwenu nendeni mkatumie mitaji hii kuwainua kimaisha na muwe mfano kwa vikundi vingine,”alisema Dk Chegeni. Aidha wakati wa mkutano wa hadhara amechangia sh milioni 10, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwa shule ya Sekondari ya Kata ambayo imepewa jina la Chegeni Secondary School kwa heshima yake na kutambua mchango mkubwa anaoutoa katika kusukuma elimu wilayani humo. Jumla ya Sekondari 18 zilianzishwa kwa msaada mkubwa kutoka kwake akiwa mbunge na hakuna kiongozi yeyote aliyefanya mak...

Wanawake Dar walizwa mamilioni na wazungu kupitia Facebook

Image
AHADI ya zawadi kubwa ikiwemo fedha na kutekwa kimapenzi kwa njia ya mtandao, kumewaliza mamia ya wanawake wa Jiji la Dar es Salaam. Watu hao wameingia katika wimbi la kutapeliwa mamilioni ya fedha na ‘wapenzi’ wao hao, wanaojitambulisha kuwa ni raia wa mataifa ya Ulaya na Marekani. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja sasa, kwa kuzungumza na wanawake watano, umebaini kuwa mamia ya wanawake wamelizwa kwa kutapeliwa fedha na wazungu hao, wanaofahamiana nao katika mtandao wa Facebook, huku wakiponzwa na ahadi za mapenzi na zawadi mbalimbali, ikiwemo fedha. Matapeli hao huwafuatilia wanawake kwenye mitandao ya kijamii hasa Facebook, ambapo huanza kwa kuwaomba urafiki na kisha kupeana namba za simu na ndipo mwanzo wa mawasiliano ya kina yanapoanza. Gazeti hili limebaini kuwa mtandao huo wa matapeli, hutumia namba mbalimbali za simu katika kuwatapeli wanawake zikiwemo namba za Ulaya, Marekani na za nchi jirani katika kuwasiliana na wale...

Mpina apiga marufuku ‘kamatakamata’ ya mifugo

Image
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku mara moja tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali katika Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na Serikali za Mitaa, kukamata mifugo holela na kutoza faini zisizo na misingi ya kisheria. Aidha amesema watendaji wa serikali waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji, hawatabaki salama, kwani serikali itawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria. Katika hatua nyingine, waziri huyo amesifu utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe katika usimamizi wenye weledi wa sheria za mifugo nchini. Mpina alitoa kauli hiyo juzi akiwa wilayani Handeni, ambapo alitumia fursa hiyo kupiga marufuku ukamataji mifugo holela huku akimtaja Gondwe kama kielelezo cha kuwa kiongozi wa kwanza kitaifa wilayani, anayezifahamu vizuri na kuzisimamia kikamilifu sheria za mifugo na kuleta tija katika ukuaji wa sekta hiyo. Alisema mbali ya kusimamia sheria, Gondwe ameweza kuanzisha kijiji cha wafu...

Baraza kuu la serikali la Libya laidhinisha rasimu ya sheria ya kura za maoni kwenye katiba

Baraza kuu la serikali la Libya limeidhinisha rasimu ya sheria ya kura za maoni kuhusu katiba. Mjumbe wa baraza hilo Bw Ali Sweih, amesema rasimu hiyo imepitishwa kwenye mkutano muhimu wa baraza hilo uliofanyika jana, na kuhudhuriwa na wajumbe 74, wajumbe 52 kati yao wamepiga kura za ndiyo. Ameongeza kuwa mchakato wa upigaji kura umefanyika kwa mujibu wa sura ya 23 ya makubaliano ya kisiasa yanayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa sura hiyo baraza kuu la serikali lenye makao yake mjini Tripoli, na baraza la chini la bunge lenye makao yake mashariki mwa nchi vinatakiwa kuunganishwa katika utungaji wa sheria hiyo ya kura za maoni kwenye katiba pamoja na sheria ya uchaguzi mkuu. Lakini bado uamuzi wa baraza kuu la serikali ya Libya, haujakubaliwa na baraza la chini la bunge.

Manowari ya Uingereza yaizuia ile ya Urusi huko North Sea

Image
Monowari ya jeshi la wa wanamaji wa Uingereza iliisindikiza ile ya Urusi katika bahari ya North Sea karibu na maji ya Uingereza siku ya Krismasi, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji wa Uingrreza. Ilisema kuwa HMS St Albans ilisindikiza Admiral Gorshkov katika sehemu zilizo karibu na maji yake. Urusi haijatamka lolote kuhusu kuhusu suala hilo. Jeshi la Uingereza lilisema kuwa kumekwa na visa hivi karibuni ambapo vyombo vya majini vya Urusi vinapita karibu na maji ya Uingereza. Mkuu wa jeshi la ulinzia nchini Uingereza Sir Stuart Peach, mapema mwezi huu alisema kuwa Uingereza na Nato wanahitaji kuweka kipaumbele suala la kulinda nyaya za mawasiliano ya mtandao zinazopiti baharini. Alisema kuwa itakuwa piga kubwa na baya kwa uchumi ikiwa nyaya hizo zinatakatwa au kuharibiwa. Nyanya hizo uunganisha sehemu tofauti za dunia kati ya nchi na mabara. Katika taarifa jeshi la majini la Uingereza lilisema kwa HMS St Albans iliitwa tarehe 23 Disemba, kupiga doria na kuifuata...

Leo ni duru ya pili ya uchaguzi wa rais Liberia kati ya George Weah na Joseph Boakai

Image
Watu nchini Liberia wanapiga kura katika duru ya pili kati ya makamu wa rais Joseph Boakai na nyota wa zamani wa kandanda George Weah. Bwana Weah, 51, alishinda duru ya kwanza lakini hakufanikiwa kupata asilimia 50 ya kura kumwezesha kuwa mshindi. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais kuchukua mahala pake Ellen Johnson Sirleaf, ilichelewa kufuatia kesi iliyokuwa mahakamani. Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili. Zaidi ya watu milioni mbili wamejiandikisha kama wapiga kura. Naye Weah, ambaye ni nyota wa zamani wa kandanda ana matumaini ya kushinnda baada ya kuwania kwa mara ya tatu. Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza mwaka 2005, lakini akashindwa wakati wa duru ya pili. Wakati wa uchaguzi ulioafuata akiwa mgombea mwenza, muungano wake ulisusia duru ya pili ukidai kuwepo udanganyifu.

Maandamano baada ya rais wa zamani wa Peru Aberto Fujimori kuachiliwa

Image
Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amemsamehe rais wa zamani Alberto Fujimori katika misingi ya kiafya katika hatua ambayo imezua maandamano makali. Fujimori, 79, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ufisadi alihamishwa kutoka gerezani kwenda hospitalini kutokana na sababu za kiafya siku ya Jumamosi. Bwana Kuczynski alikana kuwa kumsamehe kwake kulikuwa ni sehemu ya makubaliano ya chama chake kuzuia kura ya kutokuwa na imani naye. Polisi katika mji mkuu Lima walipambana na waandamanaji baada ya kuibuka kwa habari hizo. Hata hivyo wafuasi wa Fujimor ambaye aliongoza Peru kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2000 walisherehekea nje ya hospitali ya serikali ambapo alikuwa akipata matibabu. Anapendwa na baadhi ya rais wa Peru kwa kuwamaliza waasi wa Mao lakini wakosoaji wake wanamtaja kuwa mtawala wa kiimla.

JAFO APONGEZA KAMATI YA UJENZI WA MIRADI ZA VIJIJI

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amezipongeza kamati zinazosimamia ujenzi wa miradi kwa kutumia utaratibu wa ‘Force Account’ hapa nchini kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo yenye ubora na inayozingatia thamani ya fedha.   Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe ambapo alifanikiwa kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule za msingi Mitengwe, Kitonga Mango, Boga, mapoja na kituo cha Afya Maneromango.  Amesema ujenzi huo umetumia utaratibu huo wa ‘Force Account’ ambapo miundombinu mbalimbali imejengwa kwa gharama nafuu pamoja na kutoa ajira kwa mafundi wanaopatikana katika maeneo miradi hiyo inapotekelezwa.  Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kukagua jengo jipya la upasuaji, maabara, wodi ya kinamama, nyumba ya daktari, jengo la kuhifadhi maiti, vyumba 12 vya madarasa mapya, matundu ya vyoo 30, pamoja na Ofisi za walimu 3.  Mbali na hilo, Waziri Jafo ame...

Home habari MOSHI YAELEMEWA NA WINGI WA WAGENI...MIKATE,BIA,POMBE KALI VYAGOMBANIWA MOSHI YAELEMEWA NA WINGI WA WAGENI...MIKATE,BIA,POMBE KALI VYAGOMBANIWA

Image
  Mikate jana asubuhi iligeuka bidhaa adimu katika maduka makubwa mjini Moshi, kutokana na wingi wa wateja uliosababishwa na utamaduni wa wenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka walikozaliwa. Mbali ya wingi wa wageni waliorejea kusherehekea sikukuu, msongamano wa magari katikati ya mji na barabara ya njia panda ya Himo-Moshi jioni unaonekana kuvunja rekodi. Maduka makubwa ya bidhaa (supermarkets), jana asubuhi yalikuwa hayana mikate kutokana na mingi kununuliwa juzi na wenyeji wanaoenda vijijini kwa ajili ya sikukuu. Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi kati ya saa mbili asubuhi hadi saa nne uliobaini upungufu wa mikate na wasambazaji walichelewa kuisambaza. Katika baadhi ya maeneo mikate iliyokuwepo ni iliyokaa dukani kwa zaidi ya siku mbili. “Hatuna kabisa mikate, ilimalizika jana (juzi) usiku kwenye saa tatu. Wateja walikuwa wengi na kila mmoja alinunua mkate mmoja au miwili kwa ajili ya kwend...
Kampuni ya SGA Security imeadhimisha miaka 33 tangu ianze shughuli zake nchini Tanzania huku ikiwatunuku wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa muda mrefu na kupongezwa na Jeshi la Polisi kwa hatua hii. Shughuli ya kuwatambua wafanyakazi hawa ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, SACP Jumanne Muliro katika ofisi za SGA Masaki ikiwa ni moja ya majukumu yake kuhakikisha makampuni binafsi ya ulinzi na usalama yanaendeshwa kwa viwango vinavyotakiwa. Kampuni hiyi iliunda kikundi maalumu kijulikanacho kama ‘Club 20’ ambacho kinajumuisha wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20. Kwa sasa kampuni ya SGA Security imeajiri wafanyakazi zaidi ya 5,100 Tanzania na kuifanya iwe moja ya makampuni makubwa ya usalama nchini. SACP Muliro aliipongeza SGA kwa kujali masilahi ya wafanyakazi na kuongoza kwa mfano huku akisisitiza kuwa makampuni mengi ya ulinzi na usalama hayafuati utaratibu uliowekwa ikiwemo mafunzo, usimamizi na mis...

RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI

Image
Kampuni ya SGA Security imeadhimisha miaka 33 tangu ianze shughuli zake nchini Tanzania huku ikiwatunuku wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa muda mrefu na kupongezwa na Jeshi la Polisi kwa hatua hii. Shughuli ya kuwatambua wafanyakazi hawa ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, SACP Jumanne Muliro katika ofisi za SGA Masaki ikiwa ni moja ya majukumu yake kuhakikisha makampuni binafsi ya ulinzi na usalama yanaendeshwa kwa viwango vinavyotakiwa. Kampuni hiyi iliunda kikundi maalumu kijulikanacho kama ‘Club 20’ ambacho kinajumuisha wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20. Kwa sasa kampuni ya SGA Security imeajiri wafanyakazi zaidi ya 5,100 Tanzania na kuifanya iwe moja ya makampuni makubwa ya usalama nchini. SACP Muliro aliipongeza SGA kwa kujali masilahi ya wafanyakazi na kuongoza kwa mfano huku akisisitiza kuwa makampuni mengi ya ulinzi na usalama hayafuati utaratibu uliowekwa ikiwemo mafunzo, u...

TANESCO YAHIMIZA MATUMIZI BORA NA ENDELEVU YA MTO PANGANI NA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU

Image
MATUMIZI bora ya bonde la Mto Pangani, ndio njia pekee itakayosaidia kutunza vyanzo vya maji ambayo hutumika kuzalisha umeme kwenye vituo vya Pangani Hydro Systems, Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S Mahenda amewaambia wahariri wa vyombo vya habari wanaotembelea bwawa la Nyumba ya Mungu lililoko mpakani mwa wilaya ya Mwanga na Simanjiro. “Tanesco kama wadau wakubwa wa Mto huu, tumeona Mto umeingia mchanga na mchanga huo unatakiwa kuondolewa ili kuweza kuzalisha maji mengi zaidi kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu na maji hayo yaweze kupatikana kwenye vituo na hatimaye kuzalisha umeme kama ambavyo inatakiwa.” Alisema Mhandisi Mahenda. Pangani Hydro Systems ni mkusanyiko wa vituo vitatu vya kufua umeme vinavyofuatana ambavyo vimejengwa sehemu tofauti tofauti katika Mto Pangani. Vituo hivyo ni pamoja na Nyumba ya Mungu, kituo cha Hale na kituo cha New Pangani Falls na vyote kwa ujumla wake huzalisha umeme wa Megawati 97 ambazo huingizwa kwenye Gridi ya Taifa, al...

Chadema yajitosa Singida Kaskazini

Image
NI wazi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho awali kilitoa tishio la kutosimamisha wagombea katika uchaguzi wa marudio katika majimbo matatu ambayo uchaguzi utafanyika mapema mwakani, kimebadili mawazo na kusimamisha mgombea katika moja ya majimbo hayo. Uhakika wa chama hicho sasa kujitosa kupambana na wapinzani wao wakuu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) umejidhihirisha kupitia orodha ya vyama iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushiriki uchaguzi katika Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida. Katika orodha hiyo, vyama sita vya siasa, kikiwemo cha Chadema, vimepitishwa na NEC kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo hilo la Singida Kaskazini uliopangwa kufanyika Januari 13, mwakani. Hata hivyo, orodha nyingine iliyotangazwa na NEC kwa Jimbo la Longido mkoani Arusha haijamjumuisha mgombea wa Chadema na ACT Wazalendo. Uchaguzi huo pia utafanyika Januari 13, mwakani. NEC imetangaza kuwa vyama tisa vya siasa katika jimbo hilo la Longido m...

Wasomi, wanasiasa waichambua CCM

Image
WASOMI na wanasiasa nchini wameunga mkono agizo lililotolewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais John Magufuli, lililowataka viongozi wa Serikali kuwajibika mbele ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyotolewa juzi wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho, mjini Dodoma. Wakizungumza na gazeti hili, wasomi hao akiwemo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, alisema agizo hilo siyo jipya isipokuwalimekuwa halitekelezwi kutokana na kutukuwepo kwa msisitizo uliowekwa tangu nyuma katika masuala hayo ya uongozi. Alisema kutokana na uwepo wa Ilani na sera zinazosimamiwa na kila chama, hakuna ubishi kwa serikali iliyowekwa madarakani na chama chochote cha siasa, kutekeleza kile kilichopo ndani ya sera kulingana na utaratibu huo uliowekwa, na kwamba agizo hilo la Rais Magufuli limelenga kuwakumbusha viongozi hao wa serikali. “Ni kauli ya Rais, yeye pia ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa chama na msimamizi namba moja wa Ilani na sera za chama, alichokisema ...