Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka
ya kulipwa katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva
anazidi kubeba vichwa vya habari kutokana na kasi na mchango wake
anaozidi kuutoa katika klabu yake ya Difaa El Jadid.
Simon Msuva kwa mara ya pili anafanikiwa kuifungia timu yake goli
muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Morocco, Msuva jana ameipatia ushindi
wa goli 1-0 timu yake ya Difaa El Jadid dakika ya 52 dhidi ya Hassania
Agadir.
Kufunga kwa goli hilo kunamfanya Simon Msuva kusogea katika
msimamo wa ufungaji bora kwani goli dhidi ya Agadir limemfanya kutimiza
jumla ya magoli 5 na mtu anayeongoza ana magoli saba lakini huu ni
mchezo wa pili kwa Msuva kufunga mfululizo
Comments
Post a Comment