Posts

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva anazidi kubeba vichwa vya habari kutokana na kasi na mchango wake anaozidi kuutoa katika klabu yake ya Difaa El Jadid. Simon Msuva kwa mara ya pili anafanikiwa kuifungia timu yake goli muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Morocco, Msuva jana ameipatia ushindi wa goli 1-0 timu yake ya Difaa El Jadid dakika ya 52 dhidi ya Hassania Agadir. Kufunga kwa goli hilo kunamfanya Simon Msuva kusogea katika msimamo wa ufungaji bora kwani goli dhidi ya Agadir limemfanya kutimiza jumla ya magoli 5 na mtu anayeongoza ana magoli saba lakini huu ni mchezo wa pili kwa Msuva kufunga mfululizo

New York yaimarisha ulinzi katika mkesha wa mwaka mpya itakayofanyika kwenye uwanja wa Times

Idara ya polisi ya New York imeimarisha ulinzi wakati wa mkesha wa mwaka mpya utakayofanyika kwenye uwanja wa Times. Idara hiyo imesema itaongeza ulinzi nje ya uwanja huo ili kuhakikisha ulinzi dhidi ya magari kwa watu wanaosubiri kuingia kwenye eneo la ukaguzi. Aidha, polisi na washirika wengine wa usalama wataongeza idadi ya vituo vya ukaguzi kote katika uwanja wa Times ili kusimamia maeneo yanayofaa kuangalia maonyesho uwanjani hapo. Kila mwaka, karibu watu milioni mbili wanakwenda kwenye uwanja wa Times kujumuika kwenye mkesha wa mwaka mpya.

Vigogo wamiminika kurejesha fomu

Image
 IKIWA leo ndiyo siku ya mwisho kwa viongozi wa umma, kuwasilisha fomu za kuonyesha rasilimali mbalimbali walizonazo katika Ofi si za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wabunge na wakuu wa wilaya ‘wamemiminika’ katika Ofi si za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam kuwasilisha fomu hizo. Miongoni mwa viongozi waliofika na kuwasilisha fomu zao ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe; Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe; Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema; Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Harold Nsekela alisema kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa viongozi mbalimbali wanaofika katika ofisi hizo katika kanda zote na kuwasilisha fomu...

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (Tewuta) kimepongeza hatua ya Rais John Magufuli kumtaka Waziri wa Fedha kuanza uchunguzi kubaini ukweli kuhusu ubinafsishwaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Katibu Mkuu wa Tewuta, Junus Ndaro amesema chama hicho kinatambua fika kuwepo mchezo mchafu uliosababishwa na Watanzania wachache wenye uchu wa fedha wakisaidiana na wawekezaji kupora rasilimali hiyo ya Taifa. Ndaro amesema leo Alhamisi Desemba 28,2017 kuwa, kwa muda mrefu chama hicho kimekuwa kikitoa malalamiko kuhusu ufisadi huo serikalini lakini hakikusikilizwa.   “Tunampongeza Rais Magufuli kwa kuthubutu kutamka pasipo shaka kuwa taarifa alizonazo zinaonyesha kampuni ya Airtel ni mali ya TTCL, jambo hili tulilipigia kelele kwa muda mrefu,” amesema. Ndaro amesema mara zote hawakusita kutamka kuwa Celtel ambayo sasa ni Airtel ni mali ya TTCL iliyoporwa pasipo kulipwa chochote. “Wafanyakazi tunatambua ku...

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

Image
  Polisi mkoani Kilimanjaro inamshikilia mfanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF) kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Anitha Oswald (32). “Askari wakiwa doria walimkamata Anitha Oswald, ambaye ni mkazi wa Karanga, Manispaa ya Moshi, akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 216 na gramu 370 kwa kutumia gari lake analomiliki aina ya Toyota Sienta rangi ya silva,” alisema kamanda Issah. Kamanda Issah alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Majengo kwa Mtei Desemba 19 akitokea Njia Panda ya Himo kuchukua mzigo huo. “Jeshi la polisi mkoani hapa liko makini, operesheni inaendelea na hatutamvumilia mtu yeyote ambaye atabainika kujihusisha na biashara hii”, alisema. Kamanda huyo alisema polisi wanaendelea kumtafuta dereva wa gari hilo ambaye alikimbia baada ya kulitelekeza lilipogonga mti wakati akiwakimbia askari.

Shirika la ndege la Ethiopia lafikiria kuanzisha safari za kwenda Zhengzhou, China

Shirika la ndege la Ethiopia linafikiria kuanzisha safari za kwenda mji wa Zhengzhou, China. Mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya China, Mongolia, na Korea ya Kaskazini Bw Yared Berta, amesema mpango wa kuanzisha safari za kwenda mji wa Zhengzhou, Mkoani Henan China, ni sehemu ya jitihada za kuwavutia wateja wapya. Bw Berta amesema mji wa Zhengzhou ni moja ya sehemu zinazojulikana nchini China, ambao unavutia uwekezaji mwingi, na kutoa fursa kwa shirika la ndege la Ethiopia haswa kwenye huduma za uchukuzi wa mizigo. Hivi sasa Shirika la ndege la Ethiopia linasafirisha abiria 80,000 na tani 60,000 za mizigo kila mwaka kupitia miji tano ya China, ambayo ni Beijing, Hongkong, Shanghai, Chengdu na Guangzhou.

Umoja wa mataifa watoa mwito wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo yenye migogoro

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF limetoa mwito kwa pande mbalimbali zinazopambana kutekeleza wajibu wa sheria za kimataifa na kukomesha mara moja ukatili na mashambulizi dhidi ya watoto. Mkurugenzi wa miradi ya dharura wa UNICEF Bw. Manuel Fontaine amesema watoto wanalengwa na kuwekwa kwenye mazingira ya kufanyiwa ukatili mkali majumbani kwao, mashuleni na kwenye maeneo wanakocheza. UNICEF imesema watoto wamekuwa shabaha ya mstari wa mbele, na kutumiwa kama ngao, wanauawa, wanalemazwa na kuajiriwa kupigana katika sehemu mbalimbali duniani. Shirika hilo pia limesema vurugu za kingono, ndoa za lazima, utekaji nya ra na utumwa yamekuwa ni mambo ya kawaida kwenye migogoro ya Iraq, Syria, Yemen, Nigeria, Sudan Kusini na Myanmar.