RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI
Kampuni
ya SGA Security imeadhimisha miaka 33 tangu ianze shughuli zake nchini
Tanzania huku ikiwatunuku wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa
muda mrefu na kupongezwa na Jeshi la Polisi kwa hatua hii.
Shughuli
ya kuwatambua wafanyakazi hawa ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kipolisi wa Kinondoni, SACP Jumanne Muliro katika ofisi za SGA Masaki
ikiwa ni moja ya majukumu yake kuhakikisha makampuni binafsi ya ulinzi
na usalama yanaendeshwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Kampuni
hiyi iliunda kikundi maalumu kijulikanacho kama ‘Club 20’ ambacho
kinajumuisha wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka
20.
Kwa
sasa kampuni ya SGA Security imeajiri wafanyakazi zaidi ya 5,100
Tanzania na kuifanya iwe moja ya makampuni makubwa ya usalama nchini.
SACP
Muliro aliipongeza SGA kwa kujali masilahi ya wafanyakazi na kuongoza
kwa mfano huku akisisitiza kuwa makampuni mengi ya ulinzi na usalama
hayafuati utaratibu uliowekwa ikiwemo mafunzo, usimamizi na mishahara
huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa SGA.
“Ni jambo la kupongezwa sana kwa kuwa kampuni yenye wafanyakazi zaidi ya 50 walioitumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20,” alisema.
Alisema
SGA ndio ilikuwa kampuni ya kwanza ya binafsi ya ulinzi na usalama
kuanziswa Tanzania na imedhihirisha kuwa kuwajali wafanyakazi ndio
chanzo cha mafanikio.
“Nimefahaishwa kuwa wafanyakazi walioitumikia SGA kwa zaidi ya miaka kumi ni zaidi ya 1,500 jambo ambalo linastahili pongezi,” alisema
huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na
makampuni binafsi ya ulinzi na usalama kuhakikisha mkoa unakuwa salama
na kuongeza kuwa walinzi wanafanya kazi kubwa katika kuzuia ujambazi.
Naye
Mtendaji Mkuu wa SGA Group, Jules Delahaije aliupongeza uongozi wa SGA
nchini kwa kuhakikisha wafanyakazi wanaitumikia kampuni kwa muda mrefu
na pia kwa kuwatambua na kuwatunuku waliofanya kazi muda mrefu.
Aliwapa wafanyakazi hao ngao maalumu za kuonesha utumishi wao kwa zaidi ya mika 20. “Tukiwa
na wafanyakazi zaidi ya 18,000 duniani kubwa kwetu ni watu. Tumewekeza
sana katika mafunzo na pia tumehakikisha tunawalipa wafanyakazi wetu
vizuri kabisa ikilinganishwa na makampuni mengine ili tuwajengee
mazingira bora ya kazi na pia tuwe nao kwa muda mrefu,” alisema.
Mkurugenzi
Mtendaji wa SGA Tanzania Eric Sambu alisema katika miaka 33 ambayo
kampuni hiyo imefanya kazi Tanzania, imeshuhudia ukuaji mkubwa hasa
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa sababu ya mikakati
waliojiwekea na kujituma kwa wafanyakazi ili waweze kukidhi matarajio ya
wateja.
Alisema
kubwa kabisa katika mafanikio yao ni utendaji wa wafanyakazi ambao ni
waaminifu na waadilifu katika utendaji wao. “Mazingira ya sokola ndani
yametupa darasa la kutosha na imetufanya tuwawezeshe wafanyakazi wetu
ipasavyo ili waweze kukidhi matarjio ya wateja kama mazingira ya sasa
yanavyotulazimisha kufanya ambayo kwetu sasa ni jambo la kawaida
kabisa,” alisema.
“Tunaendelea
kuboresha huduma zetu na kuwekeza zaidi katika teknolojia na tumeweza
kutambuliwa katika ubora yaani ‘ISO certification on Quality Management
System’ kuanzia 2001 na hivi karibuni pia tumepokea cheti cha Afya na
Usalama yaani since ‘Occupational Health and Safety ISO 18001 Standard.’
Alisema
kampuni hiyo hadi sasa ina magari zaidi ya 224 na matawi 12 ambayo yana
ofisi zenye vifaa vya kisasa na wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kutumia
vifaa hivyo kote nchini, “ alisema Sambu.
Meneja Rasilimali Watu wa SGA Tanzania
Ebenezer Kaale, ambaye aliandaa shughuli hiyo, alisema wafanyakazi wengi
wa kampuni hiyo wanahusika na usafirishaji wa fedha, kazi ambayo
inahitaji uadilifu mkubwa na weledi. “Kwa kweli wafanyakazi
wetu wanastahili pongezi kubwa katika hili kwani tunasafirisha fedha kwa
asilimia takriban 90 ikilinganishwa na makampuni mengine ya ulinzi na
usalama,” alisema.
SGA inatoa huduma mbalimbali ikiwemo
ulinzi kwa kutumia walinzi, vifaa vya umeme, huduma za dharura,
ufuatiliaji, usafirishaji wa vifurishi na fedha.
Comments
Post a Comment