Mpina apiga marufuku ‘kamatakamata’ ya mifugo


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku mara moja tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali katika Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na Serikali za Mitaa, kukamata mifugo holela na kutoza faini zisizo na misingi ya kisheria.
Aidha amesema watendaji wa serikali waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji, hawatabaki salama, kwani serikali itawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
Katika hatua nyingine, waziri huyo amesifu utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe katika usimamizi wenye weledi wa sheria za mifugo nchini.
Mpina alitoa kauli hiyo juzi akiwa wilayani Handeni, ambapo alitumia fursa hiyo kupiga marufuku ukamataji mifugo holela huku akimtaja Gondwe kama kielelezo cha kuwa kiongozi wa kwanza kitaifa wilayani, anayezifahamu vizuri na kuzisimamia kikamilifu sheria za mifugo na kuleta tija katika ukuaji wa sekta hiyo.
Alisema mbali ya kusimamia sheria, Gondwe ameweza kuanzisha kijiji cha wafugaji, kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi na kutoa huduma bora za mifugo wakati wote.
Akizungumzia tatizo hilo la ukamataji holela wa mifugo nchini, Waziri Mpina alisema kama sekta hiyo isingekuwa inazalisha mazao ya mifugo na serikali kuamua kuagiza kutoka nje ya nchi, basi ingezilazimu kutumia Sh trilioni 17.8, lakini alisema kaya milioni 4.49 nchini zinajishughulisha na ufugaji mifugo aina mbalimbali.
“Watendaji wa serikali waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji hawatabaki salama, tutawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria,” alisema. Alisema Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002 Kifungu cha 26, inazuia mifugo kuingia kwenye hifadhi za misitu ya kitaifa au iliyo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo pamoja na wafugaji kuvunja sheria hiyo, bado wanahitaji kutendewa inavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuweka ulinganifu wa Watanzania wote mbele ya sheria za nchi.
Alibainisha kuwa kumekuwa na mazoea ya ukamataji holela wa mifugo, yanayoendelea nchini ambayo yanatekelezwa bila kuzingatia Sheria ya Ustawi wa Wanyama Na.19 ya mwaka 2008 na Kanuni zake za mwaka 2010 Kifungu cha 7 na 8 na Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Na. 17 ya mwaka 2003.
Hivyo, alisema mifugo imekuwa ikishikiliwa kama kidhibiti kwa muda mrefu na mingine kufa kutokana na magonjwa na ukosefu huduma ikiwemo matibabu, chanjo na kuogeshwa ili kuepuka magonjwa ndorobo na kupe.
“Mfano mifugo iliyomatwa Pori la Akiba la Swagaswaga mwezi Septemba hadi Desemba 13 huku ng’ombe 197 kati 411 walikufa kutokana na matatizo ambayo yangeweza kuepukika.
“Pia katika Pori la Akiba Rukwa mifugo iliyokamatwa tangu Machi 25, 2016 ilikuwa 1,332, ng’ombe waliokufa ni 692 waliobaki ni 640 tu kufikia Novemba 2017,” alisema. Alisema katika eneo la hifadhi ya wanyamapori, jumla ya mifugo 2,456 walioshikiliwa kwa miezi 3, ng’ombe 151 walikufa kufikia Novemba mwaka huu na mifugo mingine kupotea na kuuzwa bila utaratibu, jambo alilosema ni lazima lifike mwisho.
Mpina alisema mazoea hayo, kwa upande mwingine yameonesha tofauti ya namna wanajamii wanavyoshughulikiwa na sheria. Alitoa mfano wananchi waliokiuka Sheria za Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kwa kulima, kukata miti, kujenga na kuchunga mifugo kama shughuli za kiuchumi, ni wale wenye mifugo tu ndio ambao mali zao hukamatwa na kupigwa faini.
“Mazoea haya yanaendeshwa bila Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujulishwa ili kuchangia weledi na kupata uelewa wa pamoja ndani ya Serikali, hali hii inaleta mkanganyiko katika utendaji wa wizara mbalimbali ndani Serikali,” alisema Mpina.
Mpina alibainisha kuwa katika eneo la utozaji wa faini, kuna baadhi ya maeneo ambapo operesheni za wafugaji zimekuwa zikifanyika huku watendaji wa serikali wakidhani kuwa faini zilizoainishwa kwa mujibu wa sheria ni ndogo, hivyo kupanga viwango wanavyoona vinakidh

Comments

Popular posts from this blog

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA