Umoja wa mataifa watoa mwito wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo yenye migogoro



Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF limetoa mwito kwa pande mbalimbali zinazopambana kutekeleza wajibu wa sheria za kimataifa na kukomesha mara moja ukatili na mashambulizi dhidi ya watoto.
Mkurugenzi wa miradi ya dharura wa UNICEF Bw. Manuel Fontaine amesema watoto wanalengwa na kuwekwa kwenye mazingira ya kufanyiwa ukatili mkali majumbani kwao, mashuleni na kwenye maeneo wanakocheza.
UNICEF imesema watoto wamekuwa shabaha ya mstari wa mbele, na kutumiwa kama ngao, wanauawa, wanalemazwa na kuajiriwa kupigana katika sehemu mbalimbali duniani. Shirika hilo pia limesema vurugu za kingono, ndoa za lazima, utekaji nyara na utumwa yamekuwa ni mambo ya kawaida kwenye migogoro ya Iraq, Syria, Yemen, Nigeria, Sudan Kusini na Myanmar.

Comments

Popular posts from this blog

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA