Maandamano baada ya rais wa zamani wa Peru Aberto Fujimori kuachiliwa
Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski
amemsamehe rais wa zamani Alberto Fujimori katika misingi ya kiafya
katika hatua ambayo imezua maandamano makali.
Fujimori, 79, ambaye
anatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa ukiukaji wa haki za binadamu
na ufisadi alihamishwa kutoka gerezani kwenda hospitalini kutokana na
sababu za kiafya siku ya Jumamosi.
Bwana Kuczynski alikana kuwa
kumsamehe kwake kulikuwa ni sehemu ya makubaliano ya chama chake kuzuia
kura ya kutokuwa na imani naye.
Polisi katika mji mkuu Lima walipambana na waandamanaji baada ya kuibuka kwa habari hizo.
Hata
hivyo wafuasi wa Fujimor ambaye aliongoza Peru kuanzia mwaka 1990 hadi
mwaka 2000 walisherehekea nje ya hospitali ya serikali ambapo alikuwa
akipata matibabu.
Anapendwa na baadhi ya rais wa Peru kwa kuwamaliza waasi wa Mao lakini wakosoaji wake wanamtaja kuwa mtawala wa kiimla.
Comments
Post a Comment