Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita nchini Jamhuri ya Kongo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza
kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali ya Jamhuri
ya Kongo na kundi la upinzani linaloongozwa na Pastor Ntumi.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Stephane
Dujarric, inasema katibu mkuu anaelezea matumaini kwamba makubaliano
hayo yanasaidia kuleta utatuzi wa amani na endelevu wa vita katika eneo
la Pool la nchi hiyo na kupunguza msukosuko wa kibinadamu huko. Eneo la
Pool la nchi hiyo ni eneo la kusini linaliozalisha mafuta ikiwa ni
pamoja na mji mkuu Brazzaville. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko
tayari kusaidia pande hizo mbili kutekeleza makubaliano hayo.
Comments
Post a Comment