Chegeni aanza kutoa 'tiba' ya vyuma kukaza
MBUNGE wa Jimbo la Busega Dk. Raphael Chegeni amewataka vijana na
akina mama jimboni Busega kuacha kubweteka na kudai vyuma vimekaza bali
waongeze bidii kwa kuchapa kazi kwa nafasi ya kila mtu mmoja mmoja na
ndani ya vikundi vyao.
Ushauri huo ameutoa wakati akikabidhi vifaa vya kumwagilia maji
mashambani kwa ajili ya kikundi cha vijana wa Hapa Kazi Tu Busega cha
Nyanhanga na fedha taaslimu shs Milioni 1, kwa kikundi cha Inuka mama
cha Nyashimo.
“Hii ni changamoto kwenu nendeni mkatumie mitaji hii kuwainua
kimaisha na muwe mfano kwa vikundi vingine,”alisema Dk Chegeni. Aidha
wakati wa mkutano wa hadhara amechangia sh milioni 10, kwa ajili ya
ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwa shule ya Sekondari ya Kata
ambayo imepewa jina la Chegeni Secondary School kwa heshima yake na
kutambua mchango mkubwa anaoutoa katika kusukuma elimu wilayani humo.
Jumla ya Sekondari 18 zilianzishwa kwa msaada mkubwa kutoka kwake
akiwa mbunge na hakuna kiongozi yeyote aliyefanya makubwa upande wa
elimu ukilinganisha na yeye. Wilaya ya Busega inakabiliwa na upungufu wa
madarasa kwa wanafunzi 1,209 kwa mwaka ujao wa masomo.
Dk. Chegeni amewataka wananchi na wadau wote kujitoa kutekekeza
upatikanaji wa vyumba hivyo. Aidha amempongeza Rais Dk. John Magufuli
kwa hatua ya serikali yake kuwajali watoto wanyonge wa kitanzania kwa
kutoa elimu bure kwa darasa la kwanza hadi kidato cha nne na kuwataka
wananchi kuunga mkono jitihada hizo za Rais.
Comments
Post a Comment