Kampuni ya SGA Security imeadhimisha miaka 33 tangu ianze shughuli zake nchini Tanzania huku ikiwatunuku wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa muda mrefu na kupongezwa na Jeshi la Polisi kwa hatua hii.
Shughuli ya kuwatambua wafanyakazi hawa ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, SACP Jumanne Muliro katika ofisi za SGA Masaki ikiwa ni moja ya majukumu yake kuhakikisha makampuni binafsi ya ulinzi na usalama yanaendeshwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Kampuni hiyi iliunda kikundi maalumu kijulikanacho kama ‘Club 20’ ambacho kinajumuisha wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20.
Kwa sasa kampuni ya SGA Security imeajiri wafanyakazi zaidi ya 5,100 Tanzania na kuifanya iwe moja ya makampuni makubwa ya usalama nchini.
SACP Muliro aliipongeza SGA kwa kujali masilahi ya wafanyakazi na kuongoza kwa mfano huku akisisitiza kuwa makampuni mengi ya ulinzi na usalama hayafuati utaratibu uliowekwa ikiwemo mafunzo, usimamizi na mishahara huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa SGA.

Comments

Popular posts from this blog

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA