New York yaimarisha ulinzi katika mkesha wa mwaka mpya itakayofanyika kwenye uwanja wa Times
Idara ya polisi ya New York imeimarisha ulinzi wakati wa mkesha wa mwaka mpya utakayofanyika kwenye uwanja wa Times.
Idara hiyo imesema itaongeza ulinzi nje ya uwanja huo ili
kuhakikisha ulinzi dhidi ya magari kwa watu wanaosubiri kuingia kwenye
eneo la ukaguzi.
Aidha, polisi na washirika wengine wa usalama wataongeza idadi ya
vituo vya ukaguzi kote katika uwanja wa Times ili kusimamia maeneo
yanayofaa kuangalia maonyesho uwanjani hapo.
Kila mwaka, karibu watu milioni mbili wanakwenda kwenye uwanja wa Times kujumuika kwenye mkesha wa mwaka mpya.
Comments
Post a Comment