UNHCR yawarudisha wakimbizi wa Somalia 74,141 kutoka Kenya


 Image result for WAKIMBIZI SOMALIA

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema hadi kufikia tarehe 15 Novemba limewarudisha wakimbizi 74,141 wa Somalia kutoka Kenya, tangu kazi ya kuwarudisha kwa hiari ianze miaka mitatu iliyopita.
UNHCR inasema mwaka huu wakimbizi 32,478 wamesaidiwa kurudi nyumbani , na wakimbizi wapatao 71,792 kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaskazini mashariki mwa Kenya wamerudi Somalia chini ya mfumo huo wa kurudi kwa hiari tangu tarehe 8 Desemba mwaka 2014. Pia limethibitisha kuwa njia ya kuwarudisha wakimbizi kwa barabara imeanzishwa tena, ingawa barabara nchini Somalia hazipitiki kutokana na mvua mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA