Polisi Kenya wavamia shule ya Kiislamu na kuwakamata walimu 2
Polisi walisema shule hiyo iliyo katika eneo la Likoni, kusini mwa
mji wa bandari wa Mombasa, kama kituo cha kuwafunza vijana wa kiume na
watoto itikadi na uanamgambo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, chanzo cha polisi ambacho
kimehojiwa kwa misingi ya kutotajwa jina kimesema, “sehemu hiyo ilikuwa
ikifuatiliwa kwa muda mrefu.” Msemaji wa polisi Kenya hakupatikana
kutoa maoni yake.
Kiongozi mmoja wa kiislamu katika eneo hilo alithibitisha kuwepo kwa
operesheni hiyo lakini amesema hakuna ushahidi wa harakati zozote ambazo
ni kinyume cha sheria.
“Kundi la maafisa wa polisi wa ndani na wa kigeni lilivamia madrasa
ambako wanafunzi walikuwa wamelala wakati huo na kuwachukua waalimu
wao,” Sheikh Hassan Omar, afisa mwandamizi wa baraza la Maimamu na
Wahubiri Kenya (CIPK), taasisi mwamvuli ya viongozi wa dini Kenya,
aliwaambia wanahabari mjini Mombasa.
“kuna tarkiban wanafunzi 100 na waalimu wanne wa madrasa ambao
wamekamatwa na kuzuiliwa kwenye makao makuu ya polisi na hakuna
anayetueleza ni uhalifu gani waliotenda,” alisema Omar.
Bado haiko bayana kwanini polisi na CIPK walitoa maelezo tofauti kuhusu idadi ya waalimu waliokamatwa.

Comments
Post a Comment