_DSC0294
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mh. Mhandisi Stella Manyanya amefungua kikao cha siku tatu mjini Dodoma kwa njia ya Mtandao (Video Conferece) huku  akiwataka wataalam katika ngazi ya Mikoa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mwanya huo kubadilishana uzoefu lakini pia kuibua fursa zilizopo katika maeneo yao katika  uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda vidogo, vyakati na vikubwa ifikapo 2025.
Akifungua kikao hicho Manyanya alisema, kupitia fursa ya Viongozi hao wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kukutana kwa njia ya Mtandao kutawezesha wote kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mikakati ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwakupena taarifa za kujua viwanda vilivyopo katika maeneo yao na maendeleo yake, lakini pia kujua maeneo yaliyotengwa mahususi kwaajili ya viwanda hivyo.
“Mkutano huu utatusaidia pia kupambanua mikakati ya kufufua viwanda vilivyokufa na namna nzuri ya kupata wawekezaji wapya” alisema Manyanya na kuongeza kwamba  lengo la mikutano hiyo nikuwa na mkakati endelevu yakujenga uwezo kwa watendaji wa Mikoa na Halmashauri kuhusu masuala ya sekta ya Viwanda, Biashara na uwekezaji.
Manyanya amesema katika awamu ya kwanza Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA), watatoa mafunzo juu usajili wa Biashara, Miliki Ubunifu sambamba na ujenzi wa uchumi wa Viwanda kama falsafa ya Mh. Rais wa awamu ya tano inavyojiapambanua kuhusu suala zima la viwanda.
Manyanya ameongeza kuwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Seleman Jafo pamoja na Waziri mwenye dhamana na Viwanda, Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, ni viongozi ambao kwa nafasi zao wameonesha nia ya dhati katika kuhakikisha azma iliyowekwa na Serikali ya awamu ya Tano inatimia.
Akihitimisha risala yake ya ufunguzi Mh. Manyanya alisema, Mikutano hiyo ni mwanzo tu, kwani wanatarajia kuwa na chombo imara yaani kuwa na Jukwaa la Uchumi wa Viwanda kama fursa ya kuendelea kuwezesha ujenzi na uendelezaji wa Viwanda Nchini, ambapo wadau watajulishwa tarehe rasmi ya uzinduzi ambao utafanywa na Mh. Waziri Mwijage.
Mkutano huo wa siku tatu kwa njia ya mtandao ulioanza tarehe 18 na kutarajiwa kumalizika 20 Desemba, 2017 umewakutanisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Elisante Ole Gabriel,  Makatibu Tawala wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Kilimnjaro, na Ruvuma, Mikoa mingine ni  Kigoma, Lindi, Singida na Pwani sambamba na wataalamu wao wa Mikoa na wale wa Halmshauri.

Comments

Popular posts from this blog

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA