MBULU WAMPONGEZA KAMOGA KWA KUFANIKISHA MAENDELEO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Bwana
Hudson Kamoga amewashukuru wananchi wa
Kijiji cha Masieda kwa kuonyesha ushirikiano katika umaliziaji wa jengo la madarasa la shule ya
msingi Umbur.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha Masieda Yasenti Lazaro amezungumza wakati
Kamoga akizindua madarasa matatu ya shule hiyo amesema wananchi wa eneo hilo
wanashukuru kwa kuwezesha umaliziaji wa jengo la madarasa la shule hiyo.
Bwana Lazaro amesema shule hiyo imeanzishwa mwaka 2014 na kusajiliwa
mwaka 2015 ina wanafunzi 335 na vyumba vinne vya madarasa.
Mwenyekiti wa Kata ya Masieda, Nicomed Nada ameshukuru Rais John Magufuli
kumteua Kamoga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwani
anawatumikia wananchi kwa kuacha alama ya maendeleo.
Bwana Kamoga amesema baada ya kuzungumza na wadau wa maendeleo, wakawezesha
fedha hizo na kufanikisha ujenzi huo wa madarasa, ambapo shilingi milioni (7) zimemalizia ujenzi huo na shilingi milioni
3 zikatumika kwenye utafiti wa maji
katika Kijiji cha Mamagi na Genda.
Comments
Post a Comment