Jenerali Chiwenga huenda akateuliwa makamu wa rais Zimbabwe
Mkuu wa jeshi la Zimbabwe anaonekana kama atakayeteuliwa kuwa makamu
wa rais baada ya serikali kutangaza Jumatatu kuwa atastaafu wakati
akingojea uteuzi mpya.
Jenerali Constantino Chiwenga aliongoza mapinduzi yaliofikisha ukingoni utawala wa miongo kadhaa wa Robert Mugabe.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, rais Emmerson Mnangagwa
amesema atajaza nafasi za manaibu wawili wa rais katika kipindi cha siku
chache zijazo.
Mnangagwa tayari ameteua maafisa wakuu wa jeshi kadhaa kwenye baraza lake la mawaziri tangu alipoapishwa kuwa rais Novemba 24.
Alimteua generali Edzai Chimonyo aliyekuwa balozi wa Zimbabwe nchini
Tanzania kuchukua nafasi ya kamanda wa jeshi la nchi kavu kutoka kwa
kamanda Phillip Sibanda anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Chiwenga.
Wakati huo huo, serikali imetangaza kustaafu kwa mkuu wa polisi
Augustine Chiruri ambaye anasemekana kuwa mshirika wa karibu wa rais wa
zamani, Robert Mugabe.
Comments
Post a Comment