Ethiopia yasema watu 78 wamefariki kutokana mgogoro wa kikabila Oromo-Somalia

Serikali ya Ethiopia imesema idadi ya watu waliouawa katika mapigano yaliyotokea hivi karibuni kati ya makabila ya Oromo na Somali imefikia 78.
Ofisa habari wa serikali ya Ethiopia Bw. Negeri Lencho amesema, mapigano hayo yaliyotokea Desemba 14 katika wilaya ya Hawi Godina na Daro Labo kwenye eneo la Hararghe Magharibi lililokaliwa na waOromia.
Amesema siku hiyo waOromo waliokuwa njiani kurudi nyumbani baada ya kuchukua msaada wa chakula, walishambuliwa ghafla na watu wenye silaha wanaodhaniwa kuwa ni Wasomali, na kusababisha vifo vya watu 29 papo hapo.

Comments

Popular posts from this blog

Nyota ya Simon Msuva yazidi kungáa katika klabu yake ya Difaa El Jadid

MFANYAKAZI WA PPF AKAMATWA AKISAFIRISHA MIRUNGI

SAKATA LA AIRTEL LAZIDI KUKOLEA....TEWUTA NAO WAIBUKA