Baraza la umoja wa mataifa kufanya mkutano wa dharura kuhusu Jerusalem baada ya azimio kupigiwa kura ya turufu
Umoja wa mataifa utaitisha mkutano maalum wa baraza la umoja huo
kuhusu Jerusalem, baada ya Marekani kuipigia kura ya turufu rasimu ya
azimio lililopendekezwa na Misri, lenye lengo la kuitaka Marekani
ibadilishe uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Mjumbe wa Palestina Bw Riyad Mansour ameeleza matumaini yake kuwa
baraza la Umoja wa mataifa litapitisha azimio la kumtaka Rais Donald
Trump wa Marekani aondoe uamuzi wa Marekani.
Si kawaida kwa umoja wa mataifa kuitisha mkutano maalum. Hatua
hii imefikiwa baada mwenyekiti wa baraza la umoja wa mataifa Bw.
Mirislav Lajack, kukutana na maofisa wa nchi za kiarabu, muda mfupi
baada ya Marekani kuipiga kura ya turufu rasimu iliyopendekezwa na
Misri, huku wajumbe wengine wote wakiipigia kura ya ndio.
Comments
Post a Comment